Baraza la usalama laongeza muda wa ofisi yake CAR

22 Disemba 2011

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa kuhudumu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kudumisha amani kwenye Jamhuri ya Afrika ya kati kwa mwaka mmoja zaidi kwa lengo la kuhakikisha kuwepo kwa mpangilio kwa kazi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini humo.

Likiongeza muda wa kuhudumu wa ofisi hiyo baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linasema lingependa kuona serikali ikibuni tume huru ya uchaguzi ambayo itaandaa chaguzi siku za baadaye.

Baraza hilo pia limetoa wito kwa serikali na makundi yaliyojihami kuheshimu mapatano ya kitaifa na mapendekezo ya mazungumzo ya kisiasa yaliyokamilika kwa 2008.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter