Haki za wanawake zisikiukwe Misri:Bachelet

22 Disemba 2011

Mkuu wa chombo cha Umoja wa Mataifa kinachochagiza masuala ya usawa wa kijinsia UN Women,  Bi Michele Bachelet ameelezea hofu yake kuhusu taarifa za mashambulizi dhidi ya waandamanaji wanawake nchini Misri ambao wanajitokeza kutekeleza haki yao ya uhuru wa kujieleza na kukusanyika.

Bi Bachelet amesema wanawake, wanaume na watoto wamekuwa wahanga wa matumizi ya nguv kupita kiasi kwa waandamanaji wa amani katika wiki nzima iliyopita na wiki hii.

Ameongeza kuwa maelfu ya wanawake ambao walikusanyika mitaani mjini Cairo kwenye uwanja wa Tahrir siku ya Jumanne walitaka kutimiza haki yao ya kidemokrasia ya kushiriki kuunda mustakhbali wa taifa lao.

Maya Morsy ni mratibu wa UN Women nchini Misri.

(SAUTI YA MAYA MORSEY)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud