Mashambulizi ya bomu Iraq yalaaniwa vikali na UM

22 Disemba 2011

Milipuko ya bomu kwenye mji mkuu wa Iraq Baghdad iliyotokea Alhamisi imelaaniwa vikali na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo.

Kwa mujibu wa duru za habari watu 63 wameuawa na wengine 185 wamejeruhiwa katika mashambulio hayo wakiwemo watoto. Martin Kobler ambaye ni mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu Iraq amesema mashambulizi ni lazima yakome endapo Iraq itataka kuwa na mustakhbali ambao watu wake wanastahili.

Amelaani mashambulizi hayo ya bomu aliyoyaelezea kuwa ni uhalifu mkubwa dhidi ya watu wa Iraq. Bwana Kobler amewataka viongozi nchini humo kushikamana na kusaidiana majukumu ya kumaliza ghasia zinazoendelea .

Pia amerejea kusema Umoja wa Mataifa utaendelea kuwasaidia watu wa Iraq na serikali yao katika juhudi za kujenga upya amani, demokrasia na matarajio ya watu wa taifa hilo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter