Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jeshi la DR Congo na MONUSCO kukabili waasi wa LRA

Jeshi la DR Congo na MONUSCO kukabili waasi wa LRA

Jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo likishirikiana na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO wameongeza udhibi wa masuala ya usalama kuanzia tarehe 18 Desemba katika mikoa 18 ya nchi hiyo.

Mikoa hiyo inafahamika kuwa katika hatari ya mashambulizi dhidi ya waasi kutoka nchini Uganda wa LRA.

Maeneo hayo ni wilyaya za Haut-Welee , Bas-Uele katika jimbo la Orientale ambako waasi wa Uganda wa LRA wanajulikana kufanya mashambulizi hasa wakati huu wa sikukuu.

Kampeni hii itaenedelea hadi Januari pili mwaka 2012. Jean Claude Luki ni mwandishi habari wa Radio ya Umoja wa Mataifa Okapi.

(SAUTI YA JEAN CLAUDE LOUKI)