Ofisi za UM Afrika Magharibi na Kati zajadili usalama

22 Disemba 2011

Ofisi za Umoja wa Mataifa za masuala ya siasa Afrika Magharibi na Afrika ya Kati zimefanya mkutano wa pamoja kujadili masuala ya vitisho vya mpakani kama uharamia kwenye ghuba ya Guinea, hali baada ya machafuko Libya kuhusu usalama wa Sahel na mashambulizi yanayotekelezwa na kundi la waasi wa Uganda Lord’s Resistance Army LRA.

Said Djinnit mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Afrika Magharibi na Abou Moussa mwakilishi wa Katibu Mkuu Afrika ya Kati wamekutana mjini Dakar Senegal katika mwanzo wa miktano mingi ya kubadilishana mawazo. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter