Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yaelezea wasi wasi wa kuharibiwa kwa kituo ya kitamaduni mjini Cairo

UNESCO yaelezea wasi wasi wa kuharibiwa kwa kituo ya kitamaduni mjini Cairo

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa lililotwikwa jukumu la kulinda utamaduni duniani limeelezea wasi wasi wake kutokana na kuripotiwa kwa ghasia kwenye mji mkuu wa Misri Cairo na kusababisha vifo vya watu 10 mwishoni mwa Juma na kuharibiwa kwa kituo cha kihistoria.

Mkurugenzi wa shirika la elimu, Sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Irina Bokova anasema kuwa kuharibiwa kwa kituo hicho ni hasara kwa taifa la Misri na dunia nzima. Bokova amesema kuwa UNESCO itatoa usaidizi kwa kukusanya , kukadiria uharibifu na kuhifadhi mambo ya kihistoria yaliyookolewa katika eneo salama.