Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua bado ni polepole katika kuzuia Malaria miongoni mwa wanawake wajawazito:ALMA

Hatua bado ni polepole katika kuzuia Malaria miongoni mwa wanawake wajawazito:ALMA

Jamii barani Afrika zinahitaji kushiriki kikamilifu katika juhudi za kuzuia malaria miongoni mwa kina mama wajawazito. Kauli hiyo imetolewa na Bi Johannah-Joy Phumaphi katibu mkuu mtendaji wa muungano wa viongozi wa Afrika kuhusu malaria, ALMA. ALMA ni muungano wa viongozi na wakuu wa nchi wa Afrika wanaoshirikiana kutokomeza vifo vitokanavyo na malaria.

Bi Phumaphi anasema watu wamepata funzo kutokana na juhudi kubwa za kutoa vyandarua vya mbu vyenye dawa ili kuzuia kuumwa na mbu.

(SAUTI YA JOHANNAH PHUMAPHI)