Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bahrain lazima ichukue hatua mara moja kuachilia wafungwa wa kisiasa:Pillay

Bahrain lazima ichukue hatua mara moja kuachilia wafungwa wa kisiasa:Pillay

 

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay Jumatano ametolea wito uongozi wa Bahrain kuchukua hatua mara moja kushughulikia hali ya kutoamiania inayozidi baina ya serikali na jumuiya za kijamii, ikiwemo kuwaachia mara moja watu wanaoshikiliwa kwa kushiri kwa maandamano ya amani.

Pillay amesema serikali ya Bahrain inahitaji kuchukua hatua mara moja za kurejesha imani, kwa kuwaachia wote waliohukumiwa kwenye mahakama za kijeshi na wale wanaosubiri kesi kwa kutekeleza haki zao za msingi za uhuru wa kujieleza na kukusanyika. George Njogopa anaarifu.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)