Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lajadili Guinea-Bissau

Baraza la Usalama lajadili Guinea-Bissau

Hali nchini Guinea-Bissau imejadiliwa Jumatano kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuleta amani nchini humo UNOGBIS inalisaidia taifa hilo la Afrika ya Magharibi kujenga amani na hali ya utulivu. Utulivu wa Ginea-Bissau moja ya mataifa masikini kabisa duniani kila wakati unakabiliwa na vitisho vya usafirishaji haramu wa watu na uhalifu wa kupangwa.

Mwakilishi wa Ginea-Bissau kwenye Umoja wa Mataifa balozi Joao Soares da Gama anasema nchi hiyo inaendelea kuhitaji msaada wa Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA JOAO SOARES DA GAMA)