Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa Katiba ya Somalia waanza Garowe Puntlant

Mkutano wa Katiba ya Somalia waanza Garowe Puntlant

 

Mkutano wa kimataifa kuhusu katiba ya Somalia umeenza jumatano mjini Garowe Puntland, na kuingia hatua nyingine ya utekelezaji wa ramani ya amani, kwa kumaliza kipindi cha mpito.

Mkutano huo ambao unahudhuriwa na Rais wa serikali ya mpito ya Somalia, kiongozi wa Puntland, Umoja wa Mataifa, wawakilishi wa jumuiya za kijamii, mashirika ya misaada na wadau wengine wa maendeleo ya Somalia.

Balozi Augustine Mahiga ni mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Somalia na ndiye anayeendesha mkutano huo.

(SAUTI YA BALOZI MAHIGA)