Kumalizika kuondoka kwa vikosi vya Marekani Iraq kutaharakisha ujenzi imara wa taifa hilo:Ban

21 Disemba 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa hatua ya kuondoka kwa vikosi vya Marekani nchini Iraq ni sawa na kusema kufunguliwa kwa ukurasa mpya katika historia ya nchi hiyo, ukurasa ambao unaleta enzi mpya.

Ban ameeleza kuwa hii ni fursa pekee kwa serikali ya Iraq na watu wake kuonyesha ulimwenui namna walivyoimarika na kukomaa kuendesha mambo yao tena kwa ufanisi mkubwa.

Katibu Mkuu huyo ameelezea namna anavyofuatilia kwa karibu hali jumla ya kisiasa nchini humo hasa wakati huu ambapo vikosi vya kigeni vikiondoka na kuashia shughuli za ulinzi na usalama mikononi mwa askari wazawa.

Katika hatua nyingine, Ban amepongeza utendaji kazi wa kamishna maalumu ya Umoja wa Mataifa kwa ajali ya Iraq UNAMI akisema kuwa imetoa mchango mkubwa kufanikisha utengamao wa taifa hilo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter