Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yaelezea kushangazwa kwake na kifungo alichopewa wakili wa haki za binadamu

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yaelezea kushangazwa kwake na kifungo alichopewa wakili wa haki za binadamu

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea kushangazwa kwake na ripoti kuwa mahakama ya moja mjini Beijing ilimpa kifungo cha miaka mitatu wakili wa haki za binadamu Gao Zhisheng baada ya kuwa chini ya uangalizi wa muda mrefu.

Siku chache kabla ya kukamilika kwa muda huo mahakama hiyo iliamua kuwa Gao atatumikia kifungo cha miaka mitano kwa kikiuka sheria alipokuwa chini ya uangalizi . Kwa muda wa miezi ishirini Gao amekuwa chini ya uangalizi mkali katika kile kinachoonekana kama kizuizi cha nyumbani.