Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauaji ya mwandishi wa habari nchini Urusi yalaaniwa na UM

Mauaji ya mwandishi wa habari nchini Urusi yalaaniwa na UM

Utawala nchini Urusi umeitaka ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kuchunguza mauaji ya mwandishi mmoja wa habari raia wa Urusi na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika. Khadzhimurad Kalamov mwanzilishi na mhariri wa gazeti moja la kila wiki la Chervonik alipigwa risasi na kuuawa kwenye Jamhuri ya Dagestan juma lililopita.

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa umelaani mauaji ya mwandishi huyo ikiyataja kama mauaji ya hivi majuzi dhidi ya waandishi habari, watetezi wa haki za binadamu na mawakili. Rupert Colville ni msemaji wa tume ya haki za binadamu ya UM.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)