Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hofu yaongezeka kwa wahamiaji wa Ethiopia waliokwama Yemen baada ya fedha za msaada kuisha:IOM

Hofu yaongezeka kwa wahamiaji wa Ethiopia waliokwama Yemen baada ya fedha za msaada kuisha:IOM

Kumekuwa na ongezeko la hofu na woga kwenye shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kuhusu hatma ya maelfu ya wahamiaji wa Kiethiopia waliokwama kwa miezi kadhaa Kaskazini mwa Yemen wakiwa katika hali mbaya, huku msaada wa fedha za kuwasaidia ukimalizika.

Tangu Novemba mwaka 2010 IOM imekuwa ikitoa msaada muhimu wa kibinadamu ikiwemo malazi, huduma za afya na fedha za kujikimu kwa maelfu ya wahamiaji hao waliokwama Yemen ambao wanataka kujerea nyumbani. Hadi sasa IOM imeshawasaidia wahamiaji 6,169 wa Ethiopia kurejea nyumbani na kuwapa fedha za kuanzia maisha.

IOM inahitaji dola milioni 2.6 kufanikisha msaada wake kama anavyofafanua Jumbe Omari Jumbe afisa habari na mawasiliano wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)