Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada yasafirishwa kwa wakimbizi Sudan Kusini

Misaada yasafirishwa kwa wakimbizi Sudan Kusini

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa UNHCR Mataifa hii leo limezindua oparesheni kubwa ya kusafirisha misaada kwenda kwa karibu wakimbizi 50,000 nchini Sudan. Jumla ya safari 18 zilifanyika hii leo kutoka Nairobi zilisafirisha tani kadha za misaada yakiwemo matandiko ya kulalia, blanketi, neti za mbu na vyombo vya jikoni.

Misaada hiyo iliwasili masaa ya asubuhi kwenye uwanja wa ndege wa Malakal ulio Sudan Kusini, uwanja ulio karibu na maeneo walio piga kambi wakimbizi hao. Safari zingine 17 zinatarajiwa kusafirisha tani 272 za misaada kutoka kwa maghala ya UNHCR miji Nairobi. Ikiwasili kwenye uwanja wa Malakal misaada hiyo itawasafirishwa kwa njia ya barabara kwenda jimbo la Upper Nile umbali wa kilomita 300 kaskazini mashariki.