Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamii ya kimataifa yafaulu katika utunzi wa misitu:FAO

Jamii ya kimataifa yafaulu katika utunzi wa misitu:FAO

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO limesema kuwa jamii ya kimataifa imekuwa na mwaka wenye mafanikio katika utunzi wa misitu na umuhimu wa kuzishirikisha jamii zinazoishi kwenye misitu katika utunzi wa misitu.

Misitu ya Borneo–Mekong na Congo inachukua asilimia 80 ya misitu yote duniani. Huku mwaka ya kimataifa wa misitu ukielekea kukamilika FAO inasema kuwa  jitihada zake za kuhakikisha kuwepo usimamizi mzuri wa misitu pamoja na kuzishirikisha jamii zinazoishi kwenye misitu zinaendelea . Afisa wa FAO Ado Ndeso anafafanua.

(SAUTI YA ADO NDESO)