Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wapata uwezo wa kulalamikia ukiukwaji wa haki za binadamu

Watoto wapata uwezo wa kulalamikia ukiukwaji wa haki za binadamu

Watoto watakuwa na uwezo wa kupeleka malalamishi yao ya kudhulumiwa kwa shirika la kimataifa baada ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitisha itifaki kuhusu mkataba wa haki ya mtoto.

Kupitia kupitishwa kwa itifaki ya mkataba huo sasa itamwezesha mtoto kuripoti yeye binafsi kuhususiana na kukiukwa kwa haki zake zikiwemo za kuuzwa kwa watoto, dhuluma za kingono na kuwatumia watoto kama wanajeshi kwenye mizozo.

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa watoto wamefikia kiwango ya kupeleka wenyewe malalamishi kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu kwa shirika la kimatiafa. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)