Upepo mkali waua watu 950 nchini Ufilipino:UM

20 Disemba 2011

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kusafirisha misaada ili kuwasaidia maelfu ya watu walioathiriwa na upepo mkali nchini Ufilipino ambapo zaidi ya watu 950 waliuawa.

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linatoa misaada ya dharura ya chakula ili kusaidia jitihada za dharura za serikali za kutoa misaada katika eneo la Mindanao.

Msemaji wa Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF Marixie Mercado amesema kuwa shirika hilo limezindua wito wa dola milioni 4.2 ili kuweza kutoa huduma kwa watoto na wanawake walioathiriwa na upepo huo mwa muda wa miezi mitatu hadi sita kutoka sasa. Marixie Mercado anafafanua.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud