Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waitaka Syria kutekeleza mpango uliobuniwa Arab League

UM waitaka Syria kutekeleza mpango uliobuniwa Arab League

Umoja wa Mataifa umeendelea kuibana Syria kutekeleza mpango uliopendekezwa na Umoja wa nchi za kiarabu Arab League ili kutanzua mzozo unaofukuta sasa ambao umbao unatishia ustawi wa taifa hilo na wananchi wake.

Tangu kuzuka kwa vugu vugu la kutaka kuuondosha utawala wa rais Assad, mwanzoni mwanzoni mwa mwaka huu, mamia ya watu wanaripotiwa kupoteza maisha kutokana makabiliano makali toka kwa vikosi vya serikali ambavyo vinashika doria ya mbele kudhibiti maandamano ya wananchi.

Katika azimio lao la pamoja nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimesema kuwa mpango uliobuniwa na Arab League ikiwemo kuwaruhusu waangalizi wa nje kuingia nchini humo, unapaswa kutekelezwa kuanzia sasa.

Kulingana na Kamishna ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, si chini ya watu 500 wamepoteza maisha tangu kuanza kwa vugu vugu la maandamano mapema mwezi March mwaka huu.