Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waelezea shabaya yake ya kuendelea kuipiga jeki Aghanistan kukamilisha kipindi cha mpito

UM waelezea shabaya yake ya kuendelea kuipiga jeki Aghanistan kukamilisha kipindi cha mpito

Umoja wa Mataifa imeihakikishia Afghanistan kuhusu vikosi vya kulinda amani kuendelea kufanya kazi huku pia ukielezea mashirikiano yake kwa taifa hilo kuwa yasiyoyumba wala kutetereka.

Akizungumza katika Baraza la Usalama, mkuu wa operesheni ya kulinda amani ,” Hervé Ladsous ameihakikishia serikali ya Aghanistan pamoja na wanchini wake kuwa jumuiya ya kimataifa iko pamoja nao.

Amesema kuwa ili kulinda mustakaba mwema na kuimarisha mifumo ya amani na demokrasia Umoja wa Mataifa unaendelea kuweka vipaumbele vyake kwa taifa hilo na kuongeza kuwa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa vitaendelea kuweka zingatio lake hata itapofika mwishoni mwa mwaka 2014.

Ameongeza kusema kuwa ni shabaya ya Umoja wa Mataifa kuona kwamba taifa hilo linafaulu kuvuka kipindi cha mpito cha kukabidhi madaraka ya ulinzi na usalama kwa askari wa nyumbani.