Mahakama ya UM yashikilia msimamo wa kupeleka kesi ya mchungaji Rwanda

19 Disemba 2011

Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayosikiliza kesi za mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 imetupilia mbali rufaa ya mchungaji wa zamani anayeshutumiwa kuchochea mashambulizi dhidi ya raia wa Kitutsi, na kusisitiza msimamo wake wa kupeleka kesi ya mchungaji huyo kuhukumiwa kwenye mahakama ya mfuto wa taifa ya Rwanda.

Tarehe 28 Juni, mwaka huu mahakama hiyo iliyoko Arusha Tanzania ICTR ilipeleka kesi ya Bwana Uwinkindi Rwanda na kufanya kuwa ni mara ya kwanza kwa historia ya mahakama hiyo kufanya hivyo.

Rufaa ya bwana Uwinkindi ilitupiliwa mbali Ijumaa kwa majaji wa ICTR kusema wameshawishika kwamba Rwanda ina uwezo wa kukubali na kuendesha kesi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ICTR leo, rufaa ya bwana Uwinkindi imetupiliwa mbali na inashikilia msimamo wake lakini imesitisha kwa muda hatua ya kumhamishia Uwinkindi Rwanda hadi kitengo cha kesi kitakapokubali kusahihisha mashitaka dhidi ya mchungaji huyo wa zamani.

Na ICTR imesema inatumai Jamhuri ya Rwanda itadhihirisha kwa vitendo jukumu lake iliyosema kuhusu imani, uwezo na nia ya kutumia viwango vya kimataifa katika kesi zake.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter