Ban aelezea huzuni yake kufuatia kifo cha kiongozi wa DPRK

19 Disemba 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea huruma yake leo kwa mamilioni ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea DPRK wanaoomboleza kifo cha kiongozi wao Kim Jong-il aliyefariki dunia Jumamosi.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake Ban amerejea kusisitiza nia yake ya kuhakikisha amani na usalama katika rasi ya Korea akisema kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kutoa msaada kwa watu wa DPRK.

Ban ameongeza kuwa anafuatialia kwa karibu hali nchini humo. Kwa mujibu wa vyombo vya habari kiongozi huyo wa Korea amekufa kwa shinikizo la damu Desemba 17 akiwa na umri wa miaka 69, wakati alipokuwa akisafiri kwa treni nje ya mji mku Pyongyang. Amekuwa madarakani tangu mwaka 1994 kufuatia kifo cha baba yake kiongozi wa zamani wa DPRK Kim Il-Sang.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter