Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazindua muongo wa viumbe ili kuzuia kutoweka kwa familia za viumbe

UM wazindua muongo wa viumbe ili kuzuia kutoweka kwa familia za viumbe

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki–moon ametaka kuwe na urafiki kati ya ubinadamu na viumbe vingine kama moja ya njia ya kulinda manufaa yake kwa vizazi vijavyo.

Kupitia ujumbe uliosomwa kwa niaba yake na mkurugenzi wa masuala ya mawasiliano na habari Kiyo Akasaka nchini Japan wakati wa uzinduzi wa muongo wa viumbe.

Ban amesema kuwa viumbe ni muhimu katika kuendelea kuwepo kwa ubinadamu. Umoja wa Mataifa ulitaja wakati kati ya mwaka 2011 na mwaka 2020 kama muongo wa viumbe wa Umoja wa Mataifa ili kutoa mpango kuhusu viumbe na njia za kuishi pamoja kwa amani na ulimwengu.