Ban aomboleza kifo cha Rais wa zamani wa Jamhuri ya Czech

19 Disemba 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema amehuzunishwa na taarifa za kifo cha Vaclav Havel Rais wa zamani wa Jamhuri ya Czhec aliyeaga dunia Jumapili.

Katika taarifa yake Ban amesema Bwana Havel alikuwa ni sauti ya maadili kwa taifa lake wakati wa uongozi wake.

Ameongeza kuwa aliishi kwa kuzingatia ukweli jambo ambalo wengi hawakuweza kulifanya katika wakati wake na kwamba utu wake, uvumilivu na hadhi yake ulikwa ni mfano wa kigwa na wote.Ban amesema katika wakati huu wa changamoto nyingi ujasiri wake uendelee kuwachagiza wengi.

Havel aliyekuwa na umri wa miaka 75 alikuwa mwandishi na mpinzani aliyekuja kuwa Rais wa kwanza baada ya komunisti Czechoslovakia na baada ya nchi kugawika mapende Januari 1993 akawa Rais wa Jamhuri ya Czech. Ban ametoa salaam za rambirambi kwa familia ya Havel na watu wote wa Jamhuri ya Czech.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud