UNHCR yalaumu vifo vya ajali ya boti Indonesia

19 Disemba 2011

Kamishina Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Antonio Guterres ameshitushwa na vifo vya watu vilivyotokana na kuzama kwa boti iliyokuwa imejaza kupita kiasi kwenye mwambao wa Java Indonesia Jumamosi desemba 17.

Guterres amesema ni vigumu kwa mtu yoyote kutosikitishwa na idadi kubwa ya watu waliopoteza maisha katika zahma hii. Amesema kwa mwaka huu 2011 tumeshuhudia idadi kubwa ya watu kote duniani wakiweka maisha yao hatarini ili kutafuta hifadhi.

Na ameoongeza kuwa ajali hii inakuumbusha kwamba watu waliokata tama wanachukua hatua za kukatisha tama. Monica Morara na maelezo zaidi.

(RIPOTI YA MONICA MORARA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter