UNCTAD yatoa takwimu za biashara na hali ya uchumi duniani

19 Disemba 2011

Tume ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD imetoa takwimu za mwaka 2011 za utafiti wa mfumo wa biashara ya kimataifa, bei za bidhaa, usafirishaji wa majini na hali ya uchumi katika mataifa yanayoendelea.

Takwimu hizo zinaonyesha kuyumba kwa bei ya bidhaa tangu kuingia kwa milenia na pia kuchipuka kwa uchumi kwa baadhi ya nchi zinazoendelea tangu mwaka 1981 hadi 2010 mfano usafirishaji nje wa bidhjaa kutoka Uchina umekuwa kwa asilimia 8 na pato lake la taifa limeongezeka kwa karibu asilimia 7.

Takwimu zinasema katika kipindi hichohicho bidhaa zinazosafirishwa kwenda nje kutoka Marekani zimepungua kwa asilimia 3.5 na pato lake la ndani limeshuka kwa asilimia 2.5, huku mataifa ya Ulaya yakishuhudia kuanguka huduma yake ya kusafirisha nje bidhaa kwa asilimia 8 katika kipindi hichohicho. UNCTAD inasema takwimu hizi zinadhihirisha ukuaji wa uchumi wa mataifa yanayoendelea katika Nyanja ya uchumi wa kimataifa.

(SAUTI YA…..)

Takwimu hizi zimeonyesha pia kwa mwaka 2009 hadi 2010 nchi zinazoendelea ndizo zinazoshika nafasi kubwa ya usafirishaji nje bidhaa kama mafuta ya kupikia kwa asilimia 88.7 ya usafirishaji wote duniani, shaba asilimia 79 na vitu vingine kama nguo za kike, mapambo na bidhaa zilizofumwa.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud