Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban autaka uongozi wa Mpito Misri kuchukua hatua baada ya machafuko Cairo

Ban autaka uongozi wa Mpito Misri kuchukua hatua baada ya machafuko Cairo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameutaka uongozi wa mpito nchini Misri kujizuia baada ya siku kadhaa za machafuko baina ya majeshi ya usalama na waandamanaji mjini Cairo kuarifiwa kusababisha vifo vya watu 10 na kujeruhi mamia wengine.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake Ban amesema anahofia kuzaka upya kwa machafuko Cairo. Tangu Ijumaa Iliyopita waandamanaji wamemiminika tena mitaani kupinga serikali ya kijeshi ambayo iliingia madarakani mapema mwaka huu baada ya kung’olewa kiongozi wa muda mrefu madarakani Hosni Mubarak. George Njogopa anaarif.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)