Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zinazoendelea zimechagizwa kusaidiana:Ban

Nchi zinazoendelea zimechagizwa kusaidiana:Ban

Nchi zinazoendelea ambazo uchumi wake unakuwa zimechagizwa kuongeza ushirikiano kwa watoaji wa msaada wa kiuchumi kwa nchi zingine zinazoendelea.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa moja wa Mataifa Ban Ki-moon katika ujumbe maalumu wa maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa ya ushirikiano wa Kusini- Kusini inayosherehelewa kila mwaka Desemba 19.

Ban amesema siku hii imekuja katika mwisho wa mwaka alioita wa matukio ya aina yake, ulioghubikwa na maandamano maarufu dhidi ya kutokuwepo uusawa, utu na ukandamizaji.

Ushirikiano miongoni mwa nchi zinazoendelea ujulikanao kama ushirikiano wa Kusini-Kusini unaweza kusaidia kukabili changamoto za kuweka mazingira ya usawa na endelevu duniani amesema bwana Ban.

Brazil na Uchina ni mataifa mawili ambayo yanachipuuka kwa kiasi kikubwa kichumi , uchumi ambao unachukua jukumu kubwa katika ushirikiano wa Kusini-Kusini.