Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika imetolewa wito kufanya biashara na Asia

Afrika imetolewa wito kufanya biashara na Asia

Nchi za Afrika zinaambiwa kwamba kuundwa kwa ushirikiano mpya wa biashara na nchi za Asia ni moja ya njia ya kuzuia bara la Afrika kuathirika kutokana na mtikisiko wa fedha katika Ulaya.

Nchi nyingi za Afrika zina uhusiano na Ulaya kwa sababu ya ukoloni wa zamani, lakini Shirika la Fedha Duniani linatoa wito kwa bara hilo kujenga uhusiano mpya wa kibiashara.

Christine Lagarde kutoka IMF hivi karibuni atafanya ziara yake ya kwanza Africa kama Mkurugenzi Mtendaji. Atatembelea Niger na Nigeria. Amesema kupata washirika wa biashara mpya ndio njia mzuri ya kufuata.