Serikali zimetolewa wito wa kuendelea kusaidia mfuko wa Umoja wa Mataifa wa msaada wa dharura CERF

16 Disemba 2011

Serikali zimetolewa wito wa kuendelea kusaidia mfuko wa Umoja wa Mataifa wa msaada wa dharura CERF.

Mfuko huu wa dharura wa CERF ulianzishwa mwaka 2005 ili kukabiliana na hali za dharura na zinazosababishwa na migogoro duniani kote.

Nchi wanachama, sekta binafsi na watu wote huchangia mfukohuu ambao lengo lake ni dola milioni 450.

Akizungumza mwishoni mwa mkutano wa siku mbili wa ngazi ya juu mjini New York, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema fedha walizopewa CERF "wamezitumia vema".

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Tangu ilipoanzishwa miaka sita iliyopita, CERF imetoa zaidi ya dola 2 bilioni kwa mashirika ya kibinadamu kufanya kazi katika nchi na wilaya 82.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud