Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuadhimisha siku ya wahamiaji:IOM

Kuadhimisha siku ya wahamiaji:IOM

Shirika la kimataifa uhamiaji IOM linaadhimisha siku ya kimataifa ya wahamiaji Jumapili hii ambapo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa chini ya sheria za kimataifa bila ya ubaguzi au utaifa wa mtu watu wana haki ya kufurahia haki za binadamu.

IOM inasema kwamba ukosefu wa huduma za matibabu kwa wahamiaji ni za kutisha na zitahitaji kushughulikiwa kwa dharura. Huku kukiwa na zaidi ya wahamiaji milioni moja kote duniani kila nchi huwa inategemea ajira na utaalamu vyote vinavyoletwa na wahamiaji. Jumbe Omari Jumbe wa shirika la IOM anafafanua.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)