Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wajasiliamali wa Kiafrika wapata tuzo ya UM

Wajasiliamali wa Kiafrika wapata tuzo ya UM

Kampuni moja nchini Gambia ambayo imefanikiwa kuleta teknolojia ya aina yake na nyingine nchini Kenya ambayo inamilikiwa na wanawake wanaotengeneza mafuta yanayoweza kuistamilisha ngozi ni miongoni mwa kampuni zilizoshinda tuzo la Umoja wa Mataifa kutokana na mchango wake wa kusaidia maendeleo endelevu.

Kampuni hiyo ya Gambia inadaiwa kufanya mapinduzi makubwa kwa utengenezaji wa mafuta kutoka kwa zao za karanga wakati lile la Kenya lilipiga hatua kubwa kwa kuzalisha mafuta ambayo yanatoa ulinzi kwa ngozi.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP limesema kuwa makampuni hayo yameleta ubunifu unaochochea maendeleo endelevu.

Tuzo hiyo ya mwaka huu pia imeweka zingatio la pekee kwa kutambua mchango uliowekwa na wanake.