Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ocampo asisitiza haja ya kukamatwa kwa rais wa Sudan

Ocampo asisitiza haja ya kukamatwa kwa rais wa Sudan

Mwendesha mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu dhidi ya binadamu ICC amerejelea tena mwito wa kukamatwa na kufikishwa kwenye mahakama hiyo watuhumiwa wa uhalifu uliotendeka katika jimbo la Darfur ili kuleta mwanga mpya wa matumaini kwa mamilioni ya watu wanataabilka huko Sudan.

Tangu ianze kutupia jicho lake juu ya hali ya mambo huko Sudan, Mahakama hiyo imetia waranti ya kukamatwa kwa rais wa Sudan Omar al-Bashir ambaye anatuhumiwa moja kwa moja kuhusika kwenye mauwaji ya halaiki ya watu kupitia kivuli cha Janjeweeed.

Kwa mujibu wa Moreno Ocampo, kutolewa kwa waranti hiyo, kutasaidia pakubwa kumaliza uhasama na vita katika eneo la Darfur.

Mwendesha mashataka huyo amesema kama ilivyo kw anchi nyingine za afria kama Malawi, Sudani imeendelea kukaoidi agizo la mahakama ya kimataifa.