Kuna ukiukwaji wa haki za binadamu za watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na wanaobadili jinsia

15 Disemba 2011

Umoja wa Mataifa umesema ukiukwaji wa haki za watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na wale wanaobadili jinsia umekuwa ni mfumo na umesambaa duniani kote.

Hayo yameelezwa katika utafiti wa ripoti ya kwanza kabisa kuwahi kutolewa na ofisi ya kamishina wa haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa ripoti hiyo ukiukwaji wa haki za msingi za watu hao unajumuisha mauaji, ubakaji na uteswaji. Charles Radcliffe ni afisa wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa anafafanua kuhusu wanachomaanisha katika ripoti hiyo.

(SAUTI YA CHARLES RADCLIFFE)

Tunachokizungumzia hapa ni haki za binadamu za msingi duniani. Kuhakikisha kila mtu anapata haki sawa na hakuna imani yoyote ya kidini au utamaduni unaweza kuhalalisha kuwapokonya watu haki zao za msingi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter