Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikosi cha kulinda amani cha UM kuendelea kuhudumu nchini Cyprus

Kikosi cha kulinda amani cha UM kuendelea kuhudumu nchini Cyprus

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa kuhudumu kwa kikosi cha kulinda amani nchini Cyprus hadi mwezi Julai mwaka 2012 na kuutaka uongozi wa jamii za Cypriot nchini Uturuki na Ugiriki kuharakisha mazungumzo yenye lengo la kuunganisha pande hizo mbili.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukiongoza mazunguzmzo kati ya uongozi wa Cypriot nchini Uturuki na Ugiriki kwa lengo la kubuniwa kwa serikali moja ya pande mbili zilizizo na mamlaka sawa. Hata hivyo Baraza la Usalama la UM limekaribisha hatua zilizopigwa hadi sasa kwenye mazungumzo nhayo.