Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwendesha mashtaka juu ya kesi ya mauwaji ya waziri mkuu wa Lebanon Hariri asema atapumzika baada ya muhula wake kuisha

Mwendesha mashtaka juu ya kesi ya mauwaji ya waziri mkuu wa Lebanon Hariri asema atapumzika baada ya muhula wake kuisha

Mwendesha mashtaka katika mahakama iliyoundwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kufuatilia mauwaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri ameelezea nia yake ya kutoendelea kwenye wadhifa huo pale muda wake utakapokoma.

Mwendesha mashtaka huyo Daniel Bellemare, amemwarifu katibu Mkuu Ban Ki-moon kuwa hafikiri kuwania muhula mwingine kutokana na matatizo ya kiafya. Kipindi chake cha awali kuitumikia mahakama hiyo kinamalizika mwezi February mwakani, lakini sasa hatawania tena.

 Hata hivyo amesema kuwa imekuwa ni jambo la furaha na heshima kubwa kwake kuitumikia mahakama hiyo tangu kuasisiwa kwake.

Mahakama hiyo iliundwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuwahoji watuhumiwa kadhaa ambao wanadaiwa kuhusika kwenye mauwaji ya Hariri mnamo mwaka 2005.