Watoto 19,000 wa utapiamlo Djibouti:UNICEF

15 Disemba 2011

Takribani watoto 19,000 wanatibiwa kwa utapia mlo kwenye nchi ya Djibouti ambayo imekumbwa na ukame limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Shirika hilo linasema hakuna chakla cha kutosha nchini humo na kilichopo ni gharama kubwa kumudu kwa watu wengi. Mwakilishi wa UNICEF Djibouti Josefa Marrato anasema idadi ya watoto wanaotibiwa kwa utapia mlo imeongezeka kutoka 3000 mapema mwaka huu.

(SAUTI YA YUSEFA MARRATO)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud