Kiongozi wa zamani wa Khmer Rouge ambaye ni mgonjwa hatoachiliwa huru

15 Disemba 2011

Mahakama ya mauaji ya kimbari inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa nchini Cambodia imeamua kwamba Leng Thirith mwenye umri wa miaka 79, afisa wa zamani wa utawala wa Khmer Rouge ambaye alibainika kutokuwa na afya ya kumuwezesha kupanda kizimbani kwa kesi yake, sasa hatoachiliwa huru kama ilivyoamuriwa wiki iliyopita. Atasalia kizuizini.

Tarehe 17 Novemba mahakama ya Cambodia ilisema Bi Thiriti ana matatizo ya kiafya na ikaamua aachiliwe bila masharti na kesi dhidi yake isitishwe. Hata hivyo kitengo cha rufaa cha mahakama hiyo kilirhusu rufaa kwa upande wa mashitaka na kusitisha kuachiliwa kwa mshitakiwa huyo. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter