Myanmar inaongoza kwa ongezeko la kilimo cha kasumba:UNODC

15 Disemba 2011

Utafiti wa Umoja wa Mataifa uliozinduliwa Alhamisi unmeonyesha kwamba kuna ongezeko kubwa la kilimo cha kasumba Myanmar na Laos na umetoa vito wa uwekezaji mkubwa wa kufadhili aina nyingine ya mfumo wa maisha.

Utafiti huo wa kasumba Kusini Mashariki mwa Asia mwaka 2011 umetolewa mjini Bangkok Thailand na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC na unasema kilimo cha mihadarati hiyo kimepanda kutoka ekari 42,000 na kufikia karibu ekari 48,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 16 kwa mwaka 2010.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa UNODC Yuri Fedotov kupanda kwa bei ya kasumba Laos, Thailand na Myanmar kumechagiza ongezeko la kilimo cha zao hilo na hivyo ubunifu unahitajika ili kuwapa wakulima njia mbadala ya kujipatia kipato badala ya kulima kasumba. Kilimo cha kasumbu kimeongezeka mara mbili Kusini Mashariki mwa Asia tangu mwaka 2006 na Myanmar ikiwa inachukua asilimia 91 ya kilimo hicho na Laos asilimia 9.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter