Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama laongeza muda wa walinda amani wa UM Abyei

Baraza la Usalama laongeza muda wa walinda amani wa UM Abyei

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limeongeza muda wa kuhudumu wa jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa Abyei, jimbo linalogombewa na Sudan Kusini na Sudan Kaskazini.

Jeshi hilo pamoja na wajibu mwingine litasaidia pande hizo mbili kuzingatia utekelezaji wa makubaliano yao ya kuondoa wanajeshi katika eneo hilo.

Katika azimio lake Baraza la Usalama limeamua kwamba jeshi hilo la muda la Abyei UNISFA litazisaidia pande mbili katika masuala ya kubaini mpaka, kufanya uchunguzi, kutoa taarifa, kubadilishana habari, kushika doria na kudumisha usalama. George njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)