WFP yaonya watu zaidi ya milioni 2.5 watahitaji msaada wa chakula Sudan

15 Disemba 2011

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linaimarisha operesheni zake ili kuwasaidia watu milioni 2.7 walioa na njaa na kuathirika na vita Sudan Kusini kwa mwaka 2012.

Shirika hilo linasema uhaba wa mvua umesababisha kupanda kwa bei ya chakula kulikochochewa pia na vita, kuvurugika kwa soko kutokana na kufungwa kwa mpaka na kuongezeka kwa mahitaji ya chakula kwa sababu ya maelfu ya watu kurejea nyumbani na ongezeko la wakimbizi wa ndani. Monica Morara na taarifa kamili.

(RIPOTI YA MONICA MORARA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud