UNHCR yahitaji dola bilioni 7 katika miaka miwili ijayo

15 Disemba 2011

Mataifa wahisani wanakutana mjini Geneva alhamisi hii kutoa ahadi za msaada wa fedha kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR katika kufanikisha kazi zake za kuwasaidia wakimbizi na watu wasio na utaifa duniani.

Kwa mujibu wa msemaji wa UNHCR Adrian Edward jumla ya bajeti ya shirika hilo kwa miaka miwili ijayo ni zaidi ya dola bilioni 7, na ni bajeti ndogo ikilinganishwa na mwaka huu ambapo ilibidi iongezwe kwa sababu ya kuzuka matatizo mapya kama machafuko ya Ivory Coast, Libya, Pembe ya Afrika, Sudan na mafuriko ya Pakistan.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

Na taarifa za hivi punde kutoka kwenye mkutano huo zinasema hadi sasa wahisani wameahidi kutoa dola milioni 284 na ahadi zinaendelea kutolewa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter