Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukame unasababisha matatizo ya chakula kwa watu 60,000 Djibouti:WFP

Ukame unasababisha matatizo ya chakula kwa watu 60,000 Djibouti:WFP

Watu elfu 60,000 katika maeneo ya vijijini nchini Djibouti wanakabiliwa na upungufu wa chakula kutokana na ukame ambao umeikumba nchi hiyo tangu miaka sita iliyopita limesema shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP.

WFP inasema kwamba ingawa mvua imekuwa haitabiriki na ukame ni sehemu ya majira ya nchi hiyo ambayo ni nusu jangwa hali ya sasa sio ya kawaida.

Kwa mujibu wa Mario Touchette mwakilishi wa WFP Djibouti hali inakuwa mbaya kutokana na ukweli kwamba kwa sasa nchi hiyo inatarajia kuingiza chakula toka nje ili kukidhi mahitaji ya watu wake. Anasema nchi inaingiza zaidi ya asilimia 90 ya chakula kinachotumika nchini humo mijini na vijijini lakini ukame vijijini unaathiri moja kwa moja watu wa maeneo hayo.

Amesema hivyo matatizo ya chakula Djibouti vijijini ni kutokana na ukame lakini pia matatizo ya chakula yanayolikabili soko la kimataifa.

WFP inasema ongezeko la wakimbizi kutoka Somalia na Ethiopia kuingia Djibouti yameongeza shinikizo la mahitaji ya kibinadamu.