Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maskini zaidi ya milioni 30 India na Afrika Kusini kufaidika na huduma za bank:UNDP

Maskini zaidi ya milioni 30 India na Afrika Kusini kufaidika na huduma za bank:UNDP

Makampuni mawili yametangaza Jumatano kwamba yatatoa huduma za bank kwa watu zaidi ya milioni 30 wa kipato cha chini nchini India na Afrika ya Kusini ifikapo mwaka 2015.

Huduma hiyo itatolewa kupitia mpango wa kuchukua hatua kutimiza malengo ya bisahra BCTA, ambao ni mpango wa kimataifa unaochagiza sekta binafsi kupambana na umasikini, na unafadhiliwa na mashirika mbalimbali ya kimataifa likiwemo shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP.

Nchini India kampuni ya Vortex Engineering iko msitari wa mbele kusambaza mashine za kutolea pesa zinazotumia nishati ya jua huku Afrika ya Kusini bank ya WIZZIT imepanua wigo wa kutoa mikopo kusaidia kushughulikia matatizo ya maendeleo kama ukosefu wa fedha na mifumo ya bank kwa jamii masikini.