Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uzalishaji zaidi unahitajika katika sekta ya Mifugo:FAO

Uzalishaji zaidi unahitajika katika sekta ya Mifugo:FAO

Ripoti ya shirika la chakula na kilimo FAO iliyochapishwa Jumatano inasema ifikapo mwaka 2050 idadi kubwa ya watu duniani itakuwa inatumia theluthi mbili zaidi ya protini itokanayo na wanyama kuliko ilivyo sasa. Kwa mujibu wa FAO hali hiyo itaongeza shinikizo katika maliasili ya dunia.

Ripoti imeongeza kuwa ongezeko la idadi ya watu na ukuaji wa kipato vinachangia mfumo wa sasa wa matumizi makubwa ya protini ya wanyama katika nchi zinazoendelea. Ripoti hiyo iitwayo mifugo duniani 2011 imekadiria kuwa matumizi ya nyama yataongezeka kwa karibu asilimia 73 ifikapo mwaka 2050 huku matumizi ya bidhaa za maziwa yakipanda kwa asilimia 58.