Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya kuendelea kubeba mzigo wa wakimbizi wa Somalia:OCHA

Kenya kuendelea kubeba mzigo wa wakimbizi wa Somalia:OCHA

Serikali ya Kenya huenda ikaendelea kubeba mzigo wa kuhifadhi wakimbizi wa Kisomali mwaka ujao ingawa kambi kubwa kabisa ya wakimbizi nchini humo ya Dadaab imefrika. Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa mataifa kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA bado ni vigumu kufanya kazi Somalia kwa sabbu za hofu ya usalama kwa wafanyakazi wa misaada na imetoa ombi kwa pande husika kwenye mgogoro wa Somalia kuheshimu misingi ya kibinadamu.

Mwezi uliopita Umoja wa Mataifa uliomba Vikosi vya muungano wa Afrika Somalia AMISOM na wanamgambo wa Al-Shabaab kutowalenga raia na kuruhusu wafanyakazi wa misaada kutimiza wajibu wao. Kenya inahifadhi wakimbizi 600,000 kutoka Somalia na mapema mwaka huu ilipendekeza Umoja wa Mataifa ufungue kambi ya wakimbizi ndani ya Somalia ili kupunguza shinikizo kwenye kambi ya Dadaab.