Ban ataka kwanza usawa kabla ya kuwa na agenda ya pamoja ya maendeleo endelevu

14 Disemba 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameonya kuwa suala la kuwa na maendeleo endelevu kamwe haliwezi kufikiwa kama dunia haitashughulikia kwanza suala la uondoaji ukosekanaji wa uwiano na ameitolea mwito jumuiya ya kimataifa kuleta fikra mpya ambazo zitahakikisha zinazingatia usawa na ukweli.

Akizungumza kwenye mkutano wa kimataifa unaojalidia masuala ya maendeleo endelevu ya dunia, Ban amesisitiza kuwa ni jambo la kushangaza kuona kwamba upande mmoja wa dunia watu wake wanaendelea kutabika na hali ngumu za kimaisha kama vile kukabiliwa na matitizo yab ukosefu wa chakula ile hali upande mwingine unahubiri suala la maendeleo endelevu.

Amesema kuwa hali kama huyo haiwakilishi sura ya kweli na wala hakuna usawa wowote na hivyo ametaka kwanza mataifa kushughulikia na namna ya uondoaji ukosefu wa usawa.

Amesema kuwa ni matumaini yake mada ya namna hiyo itapewa zingatio la pekee ili hatimaye wimbo wa kuwa na maendeleo endelevu unapata waitikiaji

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter