UM unahitajika sasa kuliko wakati mwingine wowote:Ban

14 Disemba 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema dunia hivi sasa ipo katika kipindi kigumu kuwahi kushuhudiwa.

Na kwa maana hiyo Umoja wa Mataifa unahitajika sasa kuliko wakati mwingine wowote iwe ni katika masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa, amani, usalama na haki za binadamu au katika masala ya misaada ya kibinadamu.

Ban ameyasema hayo katika mkutano wake wa mwisho wa mwaka na waandishi wa habari mjini New York na kuongeza kuwa kila kitu kinabadilika na sheria na taratibu za zamani zinakiukwa na haijulikani ni sheria gani mpya au taratibu gani mpya zitakazoibuka.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ban ameongeza kuwa mwaka huu umekuwa wa mabadiliko na changamoto nyingi kuanzia Sudan, Yemen, Tuniasia, Misri, Haiti , Japan na kwingineo. Hali ya uchumi ni mbaya lakini dunia ni lazima ijitahidi kuweka uwiano baina ya bajeti na kuwasaidia walio masikini zaidi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter