Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya UM ICTR yasikiliza rufaa ya mfanyibiashara wa zamani wa Rwanda

Mahakama ya UM ICTR yasikiliza rufaa ya mfanyibiashara wa zamani wa Rwanda

Rufaa ya mfanyabiashara wa zamani wa Rwanda aliyekutwa na hatia ya makosa ya mauaji ya kimbari imesikilizwa Jumatano kwenye mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za mauaji ya Rwanda ya mwaka 1994, ICTR.

Mfanyabiashara huyo Gaspard Kanyarukiga alikuwa na hatia mwaka jana ya mauaji ya kimbari na kuhukumiwa kwenda jela miaka 30 na mahakama hiyo ya ICTR iliyoko Arusha Tanzania.

Majaji wa ICTR wamesema bwana Kanyarukiga alihusika na uhalifu wa kupanga mauaji ya Watutsi katika kanisa la Nyange wakati wa siku 100 za mauaji hayo mwaka 1994 nchini Rwanda. Na alikamatwa na uongozi wa Afrika ya Kusini mwaka 2004 na kufikishwa kwenye mahakama ya ICTR kukabili mashitaka.