Chad ilishindwa kumkamata rais Bashir:ICC

14 Disemba 2011

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imesema kuwa Chad haikutimiza wajibu wake wa kushirikiana na mahakama hiyo kwa kushindwa kumkamata na kumsalimisha  rais wa Sudan Omar al-Bashir alipofanya ziara nchini humo mwezi Agosti.

Rais Bashir anatafutwa na mahakama ya ICC kutokana a na mashtaka ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu baada ya mahakama hiyo kutangaza waranti wa kukamatwa kwake mwaka 2009 na mwezi Julai mwaka uliopita. Chini ya mkataba wa Roma mataifa ambayo yanashindwa kushirikiana na mahakama ya ICC kesi zao huwa zinawasilihwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter